Kwa awamu ya kwanza, Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe ilifanikiwa kufanya kikao cha kwanza cha baraza la biashara Octoba 18, 2016 kilichodhaminiwa na Local Goverment Climate (LiC)
Kikao hicho kilichofanyika Wilayani hapa na kuhudhuriwa na mwenyekiti wake Kanali Marco Gaguti (Mkuu wa wilaya ya Buhigwe), akiambatana na katibu wa baraza hilo (Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buhigwe Ndg Sadock Kihuriko), pamoja na wawakilishi wa LiC mkoa wa Kigoma, wawakilishi kutoka sekta mbalimbali na wajumbe wa baraza hilo.
Kikao hicho kilijadili agenda kuu nne
- Elimu ya biashara na ujasiliamali (Business and entrepreneurship Training).
- uwezekano wa kuboresha/mikakati ya kusaidia uwekezaji (access to finance/investment support stratergies).
- mikakati ya mwelekeo wa vipaumbele vya minyororo ya thamani (Stratergic direction for priority).
Mwenyekiti wa kikao cha baraza la biashara (Kanali Marco Gaguti) akifungua rasmi kikao hicho na kutoa maelezo na umuhimu wa baraza hilo hasa katika kuonesha fursa, changamoto na hata mikakati ya nini kifanyike ili kunufaika na uwepo wa baraza hilo katika kuleta manufaa ya wanabuhigwe kwa ujumla na kuboresha mapato ya Halmashauri kwa kupitia fursa za biashara.
"Mazingira Bora ya biashara kwa kukuza mapato ya ndani ya Halmashauri"
Baadhi ya wajumbe wa baraza kutoka sekta tofauti wakisikiliza agenda ya mikopo kutoka mwakilishi wa NMB Kasulu |
Agenda ya Mikakati ya mwelekeo wa vipaumbele vya minyororo ya thamani, ilijadiliwa. katika agenda hii suala la upatikanaji wa pembejeo za kilimo, kutokuwepo kwa viwanda kwa ajili ya usindikaji wa mazao yaliyo uti wa mgongo wilayani yalidaliwa na zaidi ya yote uboreshwaji wa mnada wa wilaya na majosho.
Ndg Boniface Nanda (Afisa kilimo wilaya) akifafanua suala la pembejeo na uwepo wa viwanda vya usindikaji mazo yapatikanayo katika wilaya yetu na hata namna ya kupata mitambo ya kufanyia kazi hiyo. |
|
Katika kikao hicho, wajumbe na wadau waliguswa na agenda zilizoandaliwa na mafisa biashara wa wilaya na hivyo kuwafanya washiriki vilivyo katika kikao.
Ndg Philemon Home ( mdau kutoka taasisi binafsi) akichangia agenda ya kilimo, hasa katika upatikanaji wa pembejeo na mifugo katika majosho na mnada |
Katika suala la kilimo ambamo jamii kubwa inajihusisha kwa ujumla, suala la upatikana wa pembejeo kwa bei nafuu na hata kupata mitambo/mashine za usindikaji wa baadhi ya mazao yalimwayo wilayani hapa, mdau Ayubu Fidel (sekta binafsi) hakusita kuzungumzia umuhimu na uhitaji wa vitu hivyo kwa wakulima wa wilaya ya Buhigwe mbele ya mwenyekiti Kanali Marco Gaguti na balaza lake kwa ujumla.
Ndg Ayubu Fidel Chanko (Mdau sekta binafsi) |
Suala la ukamilishwaji wa ujenzi wa kituo cha biashara (one stop business centre) nalo halikuachwa kama mengineyo katika kikao hicho na aliyewakilisha sekta binafsi wilaya ya Buhigwe Ndg Venance Kigwinya, akashauri baraza kwa kupitia usimamizi wa mwenyekiti wake kukamilisha utafiti na hata ujenzi wa kituo hicho ifikapo Januari 2017 kama ilivyoahidiwa na meneja wa LiC mkoa wa Kigoma Dr Betty Mlingi.
Ndg Venance Kigwinya, akifafanua juu ya umuhimu wa kituo hicho cha biashara kilivyo na tija kwa wafanya biashara wa wilaya ya Buhigwe |
Kwa mamlaka aliyonayo, mwenyekiti wa baraza kabla ya kufunga kikao alitoa nafasi kwa wageni toka nje ya wilaya ya Buhigwe kutoa japo neno kuhusu mjadala wa agenda za siku hiyo na ndipo Ndg Francis Peter (kutoka LiC Dodoma) akatoa hongera zake kwa mwenyekiti (Mkuu wa wilaya ya Buhigwe) Kanali Marco Gaguti kwa kuwa na timu nzuri iliyoonesha uchu na nia ya kuyatekeleza yote yaliyojadiliwa ili kutoa matunda bora kwa jamii. Mwakilishi huyo hakusita kupongeza namna agenda zilivyoandaliwa na zaidi ya yote kujali muda zaidi katika kujadili hoja hizo
Ndg Francis Peter (Akiwakilisha LiC Dodoma) |
Akihitimisha na kufanga kikao mwenyekiti wa baraza la biashara la wilaya ya Buhigwe Kanali Marco Gaguti alitoa shukrani zake kwa wageni kutoka LiC na hata wale walioalikwa kutoka sekta tofautitofauti na zaidi yayote wajumbe wa baraza hilo na kufunga kikao hicho rasmi.
Mwenyekiti wa baraza la biashara la wilaya ya Buhigwe Kanali Marco Gaguti akifunga kikao cha kwanza cha baraza la biashara wilaya ya Buhigwe |
Mwenyekiti wa baraza la biashara akiwa katika picha ya pamoja na wageni na wajumbe wa baraza zima la biashara la wilaya ya Buhigwe.