Ndg Frederick Joseph Ndahani (mkimbiza mwenge kitaifa) akikimbia na mwenge wa uhuru Kata ya Kinazi wilayani Buhigwe |
Aidha, Serikali kuu imechangia shilingi 1,819,532,975 sawa na 94% Halmashauri shilingi 14,200,000 sawa na 1%, Wahisani shilingi 87,000,000 sawa na 4% na Wananchi shilingi 25,400,000 sawa na 1% katika kufanikisha uzinduliwaji wa miradi hiyo.
Mbali na uzinduzi wa miradi hiyo, mbio za mwenge kwa mwaka 2017 zilibeba jumbe nne (4) kuu kuwafikishia wananchi
- "MADAWA YA KULEVYA" Mapambano dhidi ya madawa ya kulevya, tuwajali na kuwasikilize watoto na vijana.
- "RUSHWA" Tuungane kwa pamoja dhidi ya rushwa kwa maendeleo, amani na usalama wa Taifa letu.
- "UKIMWI" Tanzania bila maambukizi mapya, unyanyapaa na vifo vitokanavyo na UKIMWI inawezekana ifikapo mwaka 20130
- "MALARIA" Shiriki kutokomeza Malaria kabisa kwa manufaa ya jamii.
Miradi ambayo mwenge wa uhuru kwa mwaka 2017 ilizindua wilayani Buhigwe ni kama ifuatavyo:
- Mradi wa maji Katika kijiji cha Kirungu. Ujenzi wa miundo mbinu ya Maji
ya bomba katika Kijiji cha Kirungu
unaendelea kujengwa na Mkandarasi
mjenzi KAM / JUVE CONSTRUCTION LTD, ukisimamiwa na wataalamu wa maji toka ofisi
ya mhandisi wa maji Wilaya ya Kasulu na Buhigwe. Lengo kuu la Mradi ni kuwapatia wananchi wa Kirungu huduma ya maji safi na salama na ya kutosha
kwa umbali usiozidi mita 400 toka majumbani mwao kwa kuzingatia sera
ya maji ya mwaka 2002, kwa kufanya hivyo wananchi watapata muda wa ziada wa kufanya kazi
nyingine za uzalishaji mali na kujiletea
maendeleo. Katika mradi huu kazi zifuatazo zimefanyika; ujenzi wa chanzo cha maji
umekamilika kwa asilimia 95 , ujenzi wa tenki la kuhifadhia maji lenye mita za ujazo 150m3 unaendelea na umefikia
asilimia 85, njia kuu ya bomba
(4,081m) imekamilika kwa asilimia 85,njia za mitawanyo kijijini
(5,709m) imekamilika kwa asilimia 90 na Vituo vya kutekea maji 15 (double
type taps) vimejengwa na kukamilika kwa asilimia 80. Mradi wa maji wa Kijiji cha
Kirungu utakapokamilika utagharimu kiasi cha Tshs 504,788,762 (Wananchi
Tsh3,200,000/=, Halmashauri Tsh 4,000,000/=
na Serikali kuu Tsh 497,588,762)mpaka kufika hatua hii mkandarasi
ameishalipwa kiasi cha Tshs 412,839,702.20 na chanzo cha fedha hii ni
serikali kuu.
Ndg Amour Hamad Amour akiweka jiwe la msingi katika mradi wa maji kijiji cha KIRUNGU - Klabu ya Wapinga rushwa
-Shule ya Sekondari ya
Saint Mathias Mulumba. Klabu ya wapinga rushwa ya shule ya Sekondari Saint
Matius imeanzishwa mwaka 1994 ikiwa ni sera ya
Serikali ya kuwajenga vijana kimaadili. Klabu hii ina jumla ya wanachama
40 waliojiunga kwa hiari yao wenyewe na wamepewa mafunzo kuhusu maana ya
rushwa, aina za rushwa, sababu na madhara ya rushwa kwa Taifa letu. Klabu hii
ni miongoni mwa klabu kumi na tisa (19)
za shule za msingi na sekondari ambazo
zimeshaanzishwa katika Wilaya ya Buhigwe. Lengo kuu la kuanzishwa klabu
hii ni
kuelimisha jamii kuhusu maana ya rushwa,
madhara na umuhimu wa kuzuia na
kupambana na rushwa. Wanafunzi wataelimisha jamii kwa njia ya midahalo,
michoro, nyimbo, ngonjera, mashairi, maigizo na makala ikiwa ni pamoja na kutoa
taarifa za vitendo vya rushwa TAKUKURU. Kazi zinazotekelezwa ni kutoa
mafunzo kwa Vijana kwani ni rasilimali muhimu katika kuleta mabadiliko katika
jamii kwa kuwa ni wepesi wa kujifunza na
kubadilika. Wakishirikishwa ipasavyo katika mapambano dhidi ya rushwa tutajenga
jamii ya Watanzania waadilifu ambao wataichukia rushwa na maovu yote na hivyo
kuleta maendeleo. Hili litakuwa suluhisho la uhakika na la kudumu katika
kuikabili rushwa kwani mmomonyoko wa maadili ni moja ya sababu za msingi za
kuwepo kwa rushwa katika jamii.
Ndg Amour Hamad Amour, azidindua mradi wa wapinga rushwa katika shule ya sekondari ya mtakatifu Mathius Mulumba iliyopo Janda - Ujenzi wa Ofisi ya
Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Buhigwe. Ujenzi wa ofisi ya
Mkurugenzi makao makuu Wilaya ya Buhigwe umeanza mwaka 2015 ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuwa na ofisi
za utawala katika makao makuu ya wilaya
Halmashauri imepokea kiasi cha Tsh 1,200,000,000/= (Tsh 450,000,000/= kwa mwaka 2014/15 na Tsh 750,000,000/= kwa mwaka 2016/17) kwa ajili ya ujenzi wa mradi huu. Mradi huu unatekelezwa naTanzania Building Agency (TBA) ambayo ni taasisi ya Serikali. Lengo kuu la mradi huu ni kuboresha mazingira ya kiutendaji kazi ya kiutawala na kitaalamu. Aidha, Ujenzi huu utakapokamilika utapunguza tatizo la msongamano wa watumishi katika idara mbalimbali, uwepo wa ukumbi wa mikutano ambapo kwa sasa mikutano yote muhimu ikiwemo vikao vya waheshimiwa madiwani hufanyika katika darasa la shule ya Msingi Buhigwe. Kazi zilizotekelezwa hadi sasa ni Kufyatua tofali, Kuchimba msingi wa jengo.,Kumwaga zege la blinding, Kumwaga zege la msingi na Kujenga kuta hadi usawa wa lenta.
Mkimbiza mwenge kitaifa ndg Amour Hamad Amour, akiweka jiwe la msingi kwenye ofisi za mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Buhigwe. - Klabu ya kupinga dawa za Kulevya-Shule ya Sekondari Buyenzi. Kikundi hiki cha kupinga na kupambana na matumizi ya madawa ya kulevya kimeanzishwa tarehe 18 mwezi Mei 2017chenye jumla ya wananchama sitini (60) ambao ni wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Buyenzi.Shule hii ni ya kutwa yenye kitado cha kwanza hadi cha nne na ni shule yenye mchanganyiko wa jinsi. Lengo la kikundi hiki ni kupinga matumizi ya madawa ya kulevya kwa vijana na jamii kwa ujumla ikiwa ni pamoja na Kutoa ushauri kwa watumiaji wa madawa ya kulevya, Kuwa mabalozi kwa vijana wenzao kuhusiana na kupinga matumizi ya madawa ya kulevya kwa namna ya kumsaidia mtumiaji wa madawa ya kulevya ili aache kutumia.Kutoa elimu kwa kuwajengea uwezo wakutambua madhara yatokanayo na matumizi ya madawa ya kulevya. Kujenga uwezo wanafunzi namna ya kujizuia au kujiepusha na matumizi ya madawa ya kulevya. Pia kutambua adhabu kwa watu wanaojishughulisha na madawa ya kulevya. Kuelimisha jamii juu ya madhara na athari za matumizi ya madawa ya kulevya na kutoa ushauri kwa wanaotumia madawa ya kulevya. Uhaba wa vitendea kazi kama vipeperushi vya kutosha vinavyohusiana na madawa ya kulevya, limu, n.k, Hakuna ushirikiano na wadau mbalimbali wa maendeleo na hakuna fedha kwa ajili ya kuendesha huduma hii.
Ndg Amour Hamad Amour akipokea risala toka kwa mwanafunzi wa sekondari Buyenzi kabla ya kuzindua klabu yao ya upingaji dawa za kulevya. - Ujenzi wa Jengo la Utawala ,Vyoo na Madarasa Shule ya Msingi Muyama. Shule ya msingi Muyama
ilianzishwa mwaka 1954. Shule hii ina
wanafunzi 662, walimu 10, nyumba za walimu 8 na vyumba vya madarasa 6.
Mradi huu unajumuisha ujenzi wa jengo la utawala, ujenzi wa vyumba vitatu (3) vya madarasa , ukarabati wa vyumba sita (06) na ujenzi wa matundu sita (06) ya choo. Aidha mradi huu ulianza tarehe 16/02/2017 na kukamilika tarehe 15/07/2017.Lengo kuu la mradi huu ni kuboresha mazingira ya ufundishaji kutokana na ongezeko la uandikishaji wa wanafunzi wa awali na darasa la kwanza ,uhaba wa ofisi za utawala na uhaba wa matundu ya choo.Aidha ujenzi na uboreshaji wa miundombinu hii itaongeza ufanisi katika kutoa elimu bora kwa kuzingatia uwiano wa mwanafunzi na miundombinu iliyopo. Kazi zilizotekelezwa katika ujenzi wa matundu sita ya choo, ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa, jengo la utawala na ukarabati wa vyumba sita vya madarasa ni kuchimba shimo la choo ,kufyatua matofali, kusomba mawe, kukusanya kokoto na mchanga na kusomba , kujenga shimo la choo, kufunika choo , kujenga ukuta wa choo na kupaua , kujenga vyumba vya madarasa sita , kujenga jengo la utawala na ukarabati wa vyumba sita vya madarasa.Mradi huu umegharimu jumla ya Tsh. 133,200,000ambapo serikali kuu imechangia Tsh 111,000,000 na nguvu za wananchi thamani ya Tsh 22,200,000.
Ndg Amour Hamad Amour akiweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa jengo la utawala, vyoo na madarasa shule ya msingi Muyama - Matengenezo ya barabara ya Kitambuka –Mnanila Herimission. Barabara ya Munanila-Kitambuka
yenye urefu wa kilomita 4.2 inaunganisha Kijiji cha Musagara na Kitambuka.
Katika barabara hii kulikuwa kuna kipande cha kilomita 3.0 ambazo zilikuwa ni
korofi na kutopitika hasa kipindi cha masika kutokana na utelezi. Hivyo
Halmashauri iliiweka kwenye mpango wa matengenezo maalum wa kilomita 4.2 ambapo
kati ya hizo kilomita 03 ziliwekwa kifusi.Matengenezo haya maalum ya kilomita
4.2 cha barabara ya Munanila-Kitambuka yalianza 27/09/2016 na kumalizika
28/12/2016. Lengo
la matengenezo maalum ya kilomita
4.2 ni kuboresha huduma ya usafiri na mawasiliano kwa kuwezesha vyombo vya usafiri na waenda kwa miguu kuweza kufanya shughuli
za kimaendeleo pamoja na kuepusha ajali
zisizo za lazima.Kazi
zilizotekelezwa katika barabara hii kwa kipande cha 4,2 km ni pamoja na Upanuzi
wa barabara kutoka mita 4.0 mpaka upana wa mita 5.0, Uchongaji wa barabara kwa kilomita 4.2, Uwekaji wa changarawe kilomita 3.0 , kuzibua
mitaro/mifereji iliyoziba na Kufungua mifereji mipya. Mradi huu umegharimu kiasi cha
Tsh. 62,582,000 kutoka Mfuko wa
Barabara.
Barabara ya Munanila-Kitambuka, ikizinduliwa rasmi na Ndg Amour Hamad Amour (Mkimbiza mwenge kitaifa) - Ujenzi wa wodi ya Akina
Mama na Watoto zahanati
ya Kitambuka. Ujenzi wa zahanati ya Kitambuka
upo katika kata ya Mkatanga yenye jumla ya wakazi 19,241 katika
kijiji cha Kitambuka. Aidha zahanati hii ina jumla ya watumishi wane (4) akiwemo
Tabibnu Msaididi mmoja, Muuguzi mmoja, na wahudumu wa afya wawili. Lengo la mradi huu ni kutoa huduma za afya ya uzazi kwa akina
mama wajawazito waliopo katika kijiji
cha Kitambuka na kata ya Mkatanga kwa ujumla.Jengo hili litaweza kutoa huduma
ziafuatazo kulingana na sehemu za
jengo:- chumba cha kujifungulia, chumba cha kusubiria kabla ya kujifungua,
chumba cha kupumzika baada ya
kujifungua, na sehemu ya huduma ya kliniki ya baba, mama na mtoto. Kazi
zilizofanyika ni ujenzi wa Msingi, Kuta, Kupaua na umaliziaji wa jengo (Usafi wa Jengo). Gharama
ya mradi huu umegharimu kiasi cha Tsh 89,400,000
(Mchango wa wananchi
Tsh 2,400,000/= na Wahisania
ni Tsh87,000,000).
Uzinduzi wa zahanati ya Kitambuka kwa ajili ya mama, wajawazito na watoto ikizinduliwa na Ndg Amour Hamad Amour