UZINDUZI WA BENKI YA MATOFALI KWA AJILI YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KATA YA MUNZEZE WILAYA YA BUHIGWE.
Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe imezindua benki ya matofali kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya kata ya Munzeze. uzinduzi huo umefanyika julai 14, 2017 na kuhudhuriwa na afisa tawala wa wilaya Bw Peter Masindi (kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Bhigwe), mkurugenzi mtendaji wa halmashauri Bw Anosta Nyamoga, OCD wa wilaya Bw Venance Mapala na mwenyeji wao mheshimiwa Wilson Luzibira (Diwani wa kata hiyo).
Uzinduzi huo ambao ulikadiriwa kuwa na lengo la kufyatua tofali elfu kumi (10,000) kwa ajili ya umaliziaji wa kituo hicho cha afya. Viongozi hao wa wilaya wamliwasihi wananchi waendelee na moyo wa kujitowa kuleta maendeleo yao wenyewe na kuwakumbusha kuwa serikali ipo nao kukamilisha juhudi zao hizo. Zaidi ya hayo, viongozi hao wa wilaya walitoa rai kwa wananchi wa wilaya hiyo kuiga mfano wa kuigwa wa wananchi wa kata ya Munzeze kwa kile walichokifanya siku hiyo.
|
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Buhigwe Bw Anosta Nyamoga akishirikiana na wananchi wa kata ya Munzeze kuandaa udongo kwa ajili ya kufyatua tofali kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya kata ya Munzeze
|
Wananchi wa kata ya Munzeze wilayani Buhigwe wakionesha ari yao katika siku ya uzinduzi wa benki ya matofali kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya katika kata yao. |
|
|
0 comments:
Post a Comment