Kikao cha baraza la Madiwani kilianza kwa kamati kukutana
kwaajili ya kuvunja kamati hizo. Kwakuwa
hiki ni kikao cha mwisho wa mwaka na kutokana na kanunu na sharia Kabla ya
kuunda baraza jipya pamoja na kuteua Mwenyekiti Mwengine kwa mwaka wa fedha
2017/18 kamati hizo zinatakiwa zivunje ili kuteua kamati mpya pamoja na
wenyeviti wake.
Kikao hiki kilikuwa na Agenda kuu zifuatazo.
1. 1. Kufungua kikao.
2. 2. Taarifa ya utekelezaji ya Mwaka 2016/17.
3. 3. Ratiba ya vikaa vya kisheria vya Halmashauri.
4. 4. Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti.
5. 5. Mengineyo.
6. 6. Kufunga kikao.
Baada ya kuwasilishwa kwa Agenda tajwa hapo juu, Makamu
mwenyekiti Mh. Diwani Luzibila
kutoka kata Munzeze alifungua kikao kwa kusoma Dua ya kikao hicho kwa kikiombea
amani na Busara iwaongeza katika kufanya maamuzi kwaajili ya Halmashauri.
Makamu Mwenyekiti akifungua kikao kwa dua ya Pamoja. |
Wagombea katika ngazi ya Mwenyekit wa Halmashauri. |
Wagombea katika ngazi ya Makamu mwenyekti |
Baadaya ya uchaguzi
matokeo ya kura yalikuwa kama ifuatavyo:-
UPANDE WA MWENYEKITI:
JUMLA YA
KURA: 27
KURA ILIYOHARIBIKA:
1
Mh. VINANCE KIGWINYA: Alipata kura 16
Mh. MOSHI BUKEBUKE: Alipata kura
10
UPANDE WA MAKAMU
MWENYEKITI:
JUMLA YA
KURA: 27
KURA
ILIYOHARIBIKA: 1
Mh. HAMIS
LUKANKA: Alipata kura 16
Mh. PASCAL
NKEYEMBA: Alipata kura 10
Baada ya matakeo hayo Mwenyekiti alimtanga Mh. Venance Kigwinya (Diwani wa kata ya
Buhigwe) kuwa ni Mwenyekiti Mpya wa Halmashauri ya Wilaya Buhigwe.
Aidha kwa upande kwa Makamu Mwenyekiti, Mh. Hamis Lukanka ndio makamu mwenyekiti kwa Halmashauri ya Wilaya
ya Buhigwe.
Waheshimiwa Makamu Mwenyekiti na Mwenyekiti wa Wilaya ya Buhigwe Baada ya kushinda uchaguzi. |
0 comments:
Post a Comment