Wednesday 4 October 2017

Filled Under:

KIKAO MAALUM CHA BARAZA LA BIASHARA WILAYA YA BUHIGWE

Tarehe 29.09.2017 Wanakamati wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Buhigwe kwa kushirikiana na Wajumbe wa Baraza la Biashara la Wilaya sanjari na Baraza la Waheshimiwa Madiwani walikutana katika ukumbi wa CHAMPANDA wilayani humo kujadili na kupitisha ajenda kuhusu kupanua fursa za biashara na uwekezaji katika Wilaya ya BuhigweMwenyekiti wa KAMATI TENDAJI Baraza la Biashara Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Ndugu Anosta Nyamoga alifungua Kikao mnamo saa 11:45 asubuhi kwa kuanza na utambulisho wa meza kuu, ambapo aliongoza utambulisho huo kwa kuanza na yeye mwenyewe, kisha mwenyekiti TCCIA (Bw. Azaria Asheri), Meneja LIC-Kigoma (Dr. Betty Mlingi), mwakilishi TNBC ( Bw. Annosisye Mwamsiku), Katibu Tawala Wilaya ya Buhigwe (Ndg. Peter Masindi) pamoja na wajumbe wa kamati tendaji.
Wajumbe wa Baraza la Biashara Wilaya ya Buhigwe wakimsikiliza kwa makini Meneja mradi wa LIC (Dr. Betty Mlingi)

Katibu Tawala Wilaya ya Buhigwe(Ndg. Peter Masindi akifungua kikao maalumu cha Baraza la Biashara(W), ambaye pia ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Kikao hicho akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe(Mhe. Kanali Marco Kaguti)

Wajumbe wa Baraza la Biashara Wilaya ya Buhigwe wakisikiliza kwa makini maelezo kuhusu mafanikio ya Baraza hilo kutoka kwa Afisa Biashara (W) Ndg. Onesphory John

Meneja (LIC- Kigoma) alielezea umuhimu wa kujumuisha Baraza la Madiwani na wajumbe wa Baraza la Biashara ili kwamba wajadili kwa pamoja kutatua changamoto zinazokabili ukuaji wa uchumi ndani ya Wilaya. Meneja LIC- Kigoma aliongeza kwamba majadiliano baina ya Baraza la Biashara na Baraza la Madiwani yatafanya mabaraza yawe na nguvu hata mradi wa LIC ukimalizika na Baraza la Biashara liweze kujiendesha lenyewe. Waheshimiwa madiwani watapata fursa ya kujua kinachoendelea kwenye maeneo yao ikiwa ni pamoja na changamoto za kiuchumi zilizopo kwenye kata zao na utatuzi wake.
Kituo cha Biashara (One Stop Business Centre) kilichukuliwa kama mfano ambapo kilionekana kuwa kigeni kwa baadhi ya waeshimiwa madiwani kutokana na kutojua kinachojadiliwa kwenye vikao vya Baraza la Biashara Wilaya na maazimio yake. Hivyo kuletwa pamoja kwa mabaraza hayo mawili ilionekana ni muhimu ili kupisha sintofahamu zinazoweza kuibuka kutokana na kwamba Waheshimiwa Madiwani wachache ndio wanaofahamu uwepo wa Baraza la Biashara la Wilaya.


Agenda zilizo jadiliwa nikama zifuatazo:-
AJENDA 1: UFAFANUZI WA BARAZA LA BIASHARA, MUUNDO WAKE NA MAJUKUMU YA WAJUMBE NA UFAFANUZI JUU YA MRADI WA LIC.
Ajenda hii imegawanyika katika makundi makuu mawili nayo ni yafuatayo:-
  • UFAFANUZI WA BARAZA LA BIASHARA, MUUNDO WAKE NA MAJUKUMU YA WAJUMBE.

                             BARAZA LA BIASHARA TAIFA (TNBC)
Ni Sekretarieti / Chombo kilicho undwa kwa waraka wa Rais Na.1 wa mwaka 2001 na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 691 - 28 Sept 2001. Kwa lengo la kuboresha mazingira ya Biashara kwa maendeleo ya Taifa.
                                                   
  • MUUNDO WA BARAZA LA BIASHARA LA WILAYA
Kaburasha la ajenda hii limeambatanishwa kwa lengo la kuwapa wajumbe fursa ya kupitia wakati mratibu akifafanua ajenda hii
AJENDA 2: ONE STOP BUSINESS CENTRE.
Meneja mradi wa LIC mkoa wa Kigoma(Dr. Betty Mlingi) alieleleza juu ya kujengwa kwa kituo cha huduma za Biashara cha Wilaya (One Stop Business Centre) na Ufafanuzi juu ya mradi wa LIC.

Soma Zaidi>>>

0 comments:

Post a Comment