Ziara hii ilikuwa ya siku moja na kutembelea vijiji vitatu:-
- Kijiji cha Kasumo
- Kijiji cha Buhigwe
- kijiji cha Manyovu (Munanila)
Mradi wa REA 2 ulitengemea kukamilika tarehe 30/09/2016 lakini kutokana na idadi ndogo ya maombi ya umeme Mh. Waziri aliagiza kusogeza muda kwa mwezi mmoja ili kupata kutoa fursa kwa wengine kujiandikisha katika na kufanya maombi kwaajili ya kupa huduma hiyo. Kwahiyo Mradi huu utafikia kikomo mnamo tarehe 30/10/2016.
Pia alimuagiza Msimamizi wa Mradi wa REA pamoja na Meneje tanesco kwaajili ya kutoa mafunzo juu kifaa kipya kijulikanacho kwajina la Umeme tayari. Kifaa hili kinafanya kazi sawa na swichi kuu ya Umeme "Main Switch".
Faida ya kifaa hiki ni kupunguza gharama ya umeme katika kufunga wayaringi katika nyumba ya mteja.
Kifaa cha Umeme Tayari |