ZIARA YA MKUU WA MKOA MHE. BRG. (MST)
EMMANUEL E. MAGANGA KATIKA WILAYA YA BUHIGWE. tarehe 05-07/09/2016
MHE. BRG
(MST) EMMANUEL MAGANGA aliwasili katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya mnamo saa 3:20
asubuhi na kusaini vitabu vya wegeni, pamoja na zoezi hilo liliendana na
kutambulisha wakuu wa Idara pamoja na Waheshimiwa Madiwani. Baadaye alipokea
taarifa fupi ya Halmashauri ya wilaya Buhigwe kupitia kwa Afisa Mipango.
Mkuu wa Mkoa Mhe. BRG Emmanuel E Maganga (Kushoto) akisalimiana na Mhe. Elisha K Bagwanya(M/kiti wa Halmashauri ya Wilaya Buhigwe) |
Mhe Mkuu wa Mkoa Akisalimiana na Mkurugenzi Wa Halmashauri ya wilaya Buhigwe Nd. Anosta Nyamoga(Kulia mwa picha) |
Ratiba
iliendelea kwa kuanza kutembelea patakapo kuwa ofisi za makao makuu ya wilaya
ya Buhigwe pamoja na kufanya ukaguzi wa majengo hiyo pamoja na nyumba za wa watumishi wakuu, Mkuu wa Wilaya (DC),
Katibu tawala (DAS) na badhi ya nyumba za waku wa Idara
Mkuu wa Wilaya Col. Marco Elisha Gaguti(Kulia mwa PIcha) akimtambulisha Mhe. BRG. GEN (MST) Emmanual Maganga Katika Makao Makuu ya Wilaya Buhigwe |
Eng. Wa Halmashauri (wapili kulia mwa picha) akifafanua na Kumuelekeza Mhe Mkuu wa Mkoa Michoro ya jengo hilo |
Afisa Mipango wa wilaya ND. Mduma akifafanua Mradi huo Wa Ofisi za Halmashauri ilipo fikia |
Hizi ni nyumba za Wakuu wa IDARA PAMOJA NA NYUMBA ZA DC pamoja Na DAS |
Baada ya
zoezi hilo Mkuu wa Mkoa alikutana na kuzungumza na Watumishi wa Halmashauri (HQ)
pamoja na Waheshimiwa Madiwani.
M/Kiti wa Halmashauri (Mhe. Elisha K. Bagwanya) akitoa neno la Shukran kwa kutembelewa na Mkuu Mkuu Wa Mkoa |
Mkuu wa Wilaya (Col. Marco Elisha Gaguti- aliyesimama ) akimkaribisha Mkuu wa Mkoa Kwaajili ya kuhutubia Wataalam pamoja na Waheshimiwa Madiwani |
Mkuu wa Mkoa Akihutubia Waheshimiwa Madiwani pamoja na Wafanya Kazi wa Halmashauri |
Katika kikao
hicho mkuu wa Mkoa alitowa hutba fupi kwa watumishi pamoja na Waheshimiwa
Madiwani.
Alisisitiza
yafuatayo:
1. Ukusanyaji wa mapoto kwa Halmashauri
Katika hili Mhe. BRG alisisitiza juu ya ukusanyaji wa mapato pamoja na
kuboresha ukusanyi huo, huku akisisitiza juu ya 10% ya mgawanyo baada ya
ukusanyaji huo wa mapato katika mchanganuo wa 5% kwa Vijana na 5% kwa Wanawake.
Alimkumbusha Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkurugenzi mtendaji juu ya
kutenga mgawanyo huo
2. Utuzaji wa Amani katika Mkoa wetu
3. Napia alisisitiza kwa Madiwani kuwa
Milioni 50 za Mhe. Rais wa Awamu ya Tano Dr. John P Makufuli kuwa hizo pesa
zipo na wananchi wajiandaa zinakuja
4. Uhamiaji wa Haramu
Aliwakumbusha kuwa ukiumuhifadhi mhamiaji Haramu katika Mji wako (Kaya)
basi ni kosa na inatakiwa ipigwe vitwa swala hili kwa nguvu zote.
Baada ya Makikao hicho Mkuu wa Mkoa alitembelea Wodi ya Wazazi kituo cha Afya
cha Muyama.
Nakuzungumza na Wauguzi wa Wadi hiyo pamoja na Kuwatembelea Wazazi katika
wodi hiyo.
Mradi huu wa kituo cha Afya cha Muyama
ulidhaminiwa na World Vision
kwakuwajengea jengo hilo, na liliziduliwa Na Ndugu. George Jackson Mbijima Ambaye alikuwa kiongozi wa mbio za
mwenge 18/07/2016 Katika siku ya MwengeHospitali ya Mwayaya |
Mkuu Wa Mkoa Akimpongeza Miongoni mwa Wazazi walio jifungua katika Hospitali hiyo |
Baada
ya hapo MHE. MKUU Wa Mkoa alitembelea
Kata ya Kajana katik Ujenzi wa Madarasa, Nyumba na Vyoo katika shule ya
sekondari ya Nyamilambo. Alipongeza Mradi huu na kusisitiza Mkandarasi alipwe
mapema ili mradi huu upate kuisha mapema iwezekanvyo.
Mhandisi wa Wilaya pamoja Mkuu wa Mkoa |
Afisa Elimu Sekondari akitoa taarifa fupi juu ya Shule ya Nyamilambo (Bi. Macelna Mbehom) |
Moja ya Majengo ya Mradi huu wa shule |
Alikwenda kutembelea Mradi wa ufugaji Samaki katika bwawa la Wanakijiji
cha Mugera hasa kwa kikundi cha Wajasiliamali, kisha alikutana na Wananchi wa Kijiji Mugera na
kufanya Mkutano wake wa kwanza wa Hadhara katika Halmashauri ya wilaya ya
Buhigwe.
Aliongea na Wananchi nakuwasisitiza yafuatayo:
i.
Upimwajiwa
Ardhi kwaajili ya mpango mijiya kiwilaya
ii.
Ukusanyaji
wa Kodi
iii.
Kuto
kufumbia macho swala la Uhamiaji Haramu katika mkoa huu wa Kigoma
Taarifa fupi Juu ya Mradi wa Wasaki |
Mkuu wa Mkoa akipongeza Mradi wa Samaki kwa kuwazawadia kikundi hicho shiling 50,000/ kama pongezi kwao |
Mkuu Wa Mkoa Akihutubia Wananchi katika kijiji cha Mugera |
0 comments:
Post a Comment