Monday, 26 September 2016

Filled Under:

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AFANYA ZIARA KATIKA WILAYA WA BUHIGWE KUKAGUA MIRADI YA UMEME NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akipokelewa na baadhi ya watendaji kutoka katika Halmashauri ya wilaya buhigwe pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco)  mara baada ya kuwasili katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya Buhigwe.






 

Ziara hii ilikuwa ya siku moja na kutembelea vijiji vitatu:-
  •  Kijiji cha Kasumo
  • Kijiji cha Buhigwe
  • kijiji cha Manyovu (Munanila)  
Nakatika vijiji vyote alikutuna na kuzungumza na wananchi ili kupata kero zao juu ya Mradi huu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA 2).





Mradi wa REA 2 ulitengemea kukamilika tarehe 30/09/2016 lakini kutokana na idadi ndogo ya maombi ya umeme Mh. Waziri aliagiza kusogeza muda kwa mwezi mmoja ili kupata kutoa fursa kwa wengine kujiandikisha katika na kufanya maombi kwaajili ya kupa huduma hiyo. Kwahiyo Mradi huu utafikia kikomo mnamo tarehe 30/10/2016.






 Pia alimuagiza Msimamizi wa Mradi wa REA pamoja na Meneje tanesco kwaajili ya kutoa mafunzo juu kifaa kipya kijulikanacho kwajina la Umeme tayari. Kifaa hili kinafanya kazi sawa na swichi kuu ya Umeme "Main Switch".

Faida ya kifaa hiki ni kupunguza gharama ya umeme katika kufunga wayaringi katika nyumba ya mteja.
Kifaa cha Umeme Tayari


 






 

0 comments:

Post a Comment